Учебник соответствует разделу 2 (семестры 4-6) действующей обновленной Программы по языку суахили (основному) для студентов факультета международных отношений, уровень "Бакалавр"
Вид материала | Учебник |
- Программа по испанскому языку (основному) для студентов ф-та международного бизнеса, 78.34kb.
- Московский государственный институт международных отношений (университет) мид, 1816.26kb.
- Программа курса «Основы политологии» для студентов факультета международных отношений, 717.08kb.
- Государство Израиль в системе международных отношений второй половины XX века, 590.32kb.
- Томский государственный университет кафедра новой, новейшей истории и международных, 2383.42kb.
- Отделения факультета Международных отношений Отделение "Регионоведение и дипломатия", 33.05kb.
- Учебник / Под ред. А. В. Торкунова. М.: «Российская политическая энциклопедия» (росспэн), 7372.83kb.
- Программа курса "Этнополитология" для студентов факультета Политологии, 113.53kb.
- Программа подготовки аспирантов кафедры по специальности 07. 00. 15 История международных, 185.3kb.
- Рекомендации по организации видов учебной деятельности студентов Усвоение знаний, 312.97kb.
kudhibiti mazingira
Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameafiki pendekezo la baraza jipya la hifadhi na usimamizi wa mazingira kuwa zitungwe sheria kali na iundwe mahakama maalum ili kudhibiti wachafuzi wa mazingira nchini.
Pendekezo hilo lilitolewa kwa makamu wa rais na mwenyekiti wa baraza hilo jipya, alipokuwa akimkaribisha makamu wa rais kutoa hotuba ya uzinduzi wa baraza hilo. Katika hotuba ya uzinduzi huo wa baraza la hifadhi na usimamizi wa mazingira, makamu wa rais alisema kuwa serikali iko mstari wa mbele katika kutilia mkazo suala zima la mazingira na ndiyo sababu baraza hilo limewekwa chini ya ofisi yake.
Alisema sheria zilizopo kwa kiasi fulani zinatoa nafasi kwa watu kutokuwa makini lakini wakati umefika ambao zinahitajika sheria kali ili kuokoa mazingira yetu. Amelishauri baraza hilo kubuni mikakati madhubuti ya kuielemisha jamii pamoja na kubuni mbinu mbali mbali kama vile kubuni nishati nyingine badala ya ile inayotokana na miti.
Baraza hilo halina budi kutilia mkazo mikoa mingine katika utaratibu mzima wa kuielemisha jamii kuhusiana na athari zinazotokana na uchafuzi wa mazingira badala ya kutazama Dar es Salaam tu. Alizitaka taasisi zote zinazohusika na utoaji vibali kwa wawekezaji kuwa makini, kwani wawekezaji wengine wanaweza kuchangia katika kuharibu mazingira yetu hasa wale wanaowekeza katika viwanda.
“Ili kuweza kufanikisha hilo bila ya kuwabughudhi wawekezaji, ni lazima tuwe na viwango vya kimataifa vya uhifadhi na usimamizi wa mazingira”, alisema.
Makamu wa rais alilionya baraza hilo jipya kuepukana na malumbano na idara ya kuhifadhi mazingira kama ilivyokuwa katika mabaraza yaliyopita.
8. Переведите текст:
Rais apongeza upandaji miti
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewapongeza wananchi wa Mwanza kwa juhudi zao za kupanda miti kutunza mazingira.
Rais wa nchi aliye katika ziara ya siku nane mkoani Mwanza alitoa pongezi hizo juzi alipokuwa akiwahutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Misasi wilayani hapa. Alisema juhudi hizo zimekuja wakati unaofaa kwani alisema uhaba wa miti unachangia kuharibu mazingira jambo ambalo linatishia maisha ya binadamu.
Katika kutambua juhudi hizo rais aliahidi kukipatia msaada wa miche yenye thamani ya shilingi laki moja kikundi cha akina mama cha mazingira wilayani hapa kwa ajili ya kuendeleza juhudi zao za upandaji miti. Aliahidi kulipa deni la shilingi 50 elfu walilokuwa wanaidai ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza kuhusiana na mradi huo wa miche.
Rais alirudia kauli kwamba serikali yake imetumia miezi 18 ya kwanza kuweka mazingira mazuri ya uchumi, jambo ambalo alisema ni kuwahamasisha wananchi kujitegemea na kupata misaada na mikopo kutoka nje kwa ajili ya miradi mikubwa ya maendeleo nchini.
Alisema wakati anachukua madaraka wafadhili walikuwa wamegoma kutoa mikopo kwa sababu ya kutolipwa madeni yao. “Lakini kwa sababu tumeanza kulipa madeni hayo, wafadhili wamekubali kutoa mikopo,” alisema na kuongeza kwamba kuna dalili kwamba uchumi wa nchi utainuka hivi karibuni.
9. Дайте эквиваленты на суахили:
созывать сессию парламента; отважиться объявить войну браконьерам; отстаивать свою точку зрения; давать оценку последним шагам правительства; согласиться с решением заместителя министра; одобрить важное дополнение к закону; устроить митинг по случаю открытия выставки; институт, занимающийся разработкой новых видов энергии; дать согласие на проведение забастовки; бойкотировать решение суда; предоставлять долгосрочный кредит; брать взаймы.
10. Переведите:
- Проблемы защиты окружающей среды широко обсуждаются во всем мире, потому что человечество уже нанесло огромный вред природе и стоит перед выбором между жизнью и смертью.
- Меры по защите окружающей среды недостаточны, и они гораздо меньше тех, которые следовало бы принять для предотвращения ущерба.
- Развивающимся странам, сталкивающимся с нищетой, было бы гораздо легче идти вперед, если бы они в полной мере осознали необходимость оберегать окружающую среду.
- Зачастую те, кто участвует в борьбе против загрязнения природы, не понимают, что следует бороться не с последствиями, а с причинами этой беды.
- Промышленные предприятия оказывают вредное воздействие на здоровье человека, поскольку они загрязняют воздух, которым он дышит, воду, которую пьет, и землю, которую возделывает для получения пропитания.
- Некоторые люди, уничтожающие леса и использующие недра земли в неограниченном количестве, все еще думают только о сегодняшнем дне, не задавая себе вопрос, а как же будут жить будущие поколения.
- В африканских странах население из-за своей бедности все еще вынуждено корчевать деревья для получения древесины и угля на продажу, поджигать леса ради удачной охоты, ловить рыбу с помощью динамита.
Msamiati
-itisha созывать (собрание и т.п.) mahakama (-) суд, судебная
-bughudhi обижать; оскорблять инстанция
-kumba охватывать, захватывать madhubuti 1) надежный
-dhibiti 1) защищать, охранять 2) прочный, твердый
2) контролировать nishati (-) энергия
malumbano (мн.) дискуссия; kibali (vi-) согласие,
споры; перекрестный допрос одобрение
madhara (мн.) 1) вред, ущерб, baruti (-) порох
убыток 2) беда, несчастье nyongeza (-) добавление;
-kithiri увеличиваться, расти дополнение
-zindua открывать (выставку, makamu (-) заместитель
памятник), провозглашать открытым -kopa брать взаймы,
uzinduzi (ед.) [торжественное] занимать
открытие mkopo (mi-) заем; кредит
-diriki отваживаться, решаться, -toa mkopo давать кредит
осмеливаться -goma 1) бастовать
shime скорей!, вперед! 2) бойкотировать
-tia shime подбадривать mgomo (mi-) забастовка
kemikali (-) химикаты taasisi (-) институт;
-epa, -kwepa уклоняться, избегать исследовательский центр
kamambe, kabambe важный, -tathmini оценивать
значительный, первоклассный makali (мн.) острие; острота
mtazamo, mtizamo (mi-) взгляд, tathmini (-) оценка
точка зрения -afiki соглашаться, одобрять
Урок 28. Somo la ishirini na nane
(marudio)
1. Переведите письменно следующие тексты:
Mji wa zamani wenye magofu mengi
Tafiti mbalimbali kuhusu tamaduni za watu walioishi mjini Kilwa zilianza mwaka 1950, na miezi michache baadaye zilipatikana fedha za shaba zilizowahi kutumiwa na watu wa Kilwa. Pia vipande vya mavazi, shanga, madini yaliyowahi kuuzwa au kununuliwa, mikufu ya dhahabu na shaba zinazodaiwa kuvaliwa na watu wa enzi hizo.
Mwaka 1981, kisiwa hicho kiliwekwa katika kundi la maeneo yanayohifadhiwa kimataifa, huku majengo kama Msikiti mkuu, Mkutini Palace na Husuni kubwa yakiangaliwa zaidi.
Mwaka 2004, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) lilikiweka kisiwa hicho kuwa miongoni mwa yale yaliyoko hatarini kutoweka.
Kwa muda mrefu, kasi ya uharibifu wa mabaki ya majengo yaliyoko kwenye kisiwa hicho ni kubwa, na maeneo mengi ya akiolojia yamepoteza muonekano wake wa siku za nyuma. Watafiti wanaonya kuwa baada ya miaka 50 ijayo, Kilwa itashuhudiwa kupoteza hadhi yake ya karne nyingi zilizopita.
Mbali ya maeneo hayo, vivutio vingine vya kisiwa hicho ni kaburi za watawala wa kiarabu na kireno, magofu ya majengo yaliyojengwa kwa utamaduni wa kiarabu, mabaki ya misikiti iliyojengwa kwa mapaa mithili ya vyungu na kisima kikuu kisichokauka.
Hata hivyo juhudi za kuvutia watalii wa ndani na nje ya nchi haziridhishi na hii ni kutokana na miundombinu duni inayoelekea Kilwa. Kwa miaka mingi, usafiri wa barabara umekuwa kikwazo na inawezekana kumalizika kwa barabara ya lami kati ya Dar es Salaam na Lindi kukasaidia kuongeza idadi ya watu watakaokitembelea kisiwa hicho.
Sweden yakarabati jengo la kihistoria Bagamoyo
Ubalozi wa Sweden umekabidhi jengo lililokarabatiwa mjini Bagamoyo, ambalo kati ya miaka 1850 na 1900 lilikuwa likitumika kama kituo cha kupumzika wafanyabiashara kutoka sehemu mbalimbali za dunia.
Balozi wa Sweden alikabidhi jengo hilo mapema wiki hii kwa mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, mkoa wa Pwani, Grace Mesaki. Jengo hilo limefanyiwa ukarabati wa dharura kulinusuru lisianguke.
Wafanyabiashara wa bidhaa mbalimbali na watumwa walikuwa wakianzia au kumalizia safari zao katika jengo hilo la kihistoria ambalo ni miongoni mwa majengo ya zamani mjini Bagamoyo.
Miongoni mwa vitu vya kihistoria vilivyokutwa katika maeneo ya karibu na jengo hilo ni sarafu za Uingereza, shanga za Ulaya, pete na bangili za madini mbalimbali na chupa ya uturi kutoka Marekani.
Ukarabati wa jengo hilo ni sehemu ya sera ya Sweden kutumia rasilmali zake kutunza mazingira ya maeneo ya Pwani.
Katika sherehe ya kukabidhi jengo hili, ilielezwa kwamba serikali ya Tanzania kupitia wizara ya maliasili na utalii ina mpango wa kutunza majengo yote ya kihistoria yaliyomo mjini humo. Mkurugenzi wa mambo ya kale katika wizara hiyo, ambaye alihudhuria sherehe hizo, alisema tayari jina la mji wa Bagamoyo limepelekwa katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) likisubiri kuwekwa katika orodha ya miji vivutio.
2. Дайте эквиваленты на суахили:
дорогая серебряная цепочка; застегнуть цепочку на шее; выглядеть как кинозвезда; рычать наподобие льва; купить в подарок флакон духов; разбить бутылку редкого вина; развитая инфраструктура; помехи на дороге; ставить “палки в колеса”; преодолевать препятствия; ускорить реставрационные работы; восстановить разрушенное здание; охранять национальное достояние; поместить капитал в надежный банк; принять неотложные меры; делать срочный ремонт; развалины древней мечети; остатки арабских захоронений; терять свой исторический облик; непересыхающий колодец.
3. Переведите вопросы по содержанию текстов и дайте на них ответы на суахили:
1. Когда вперые археологи начали исследовать окрестности г. Килва Кисивани? 2. Что им удалось обнаружить в результате раскопок? 3. Когда Килва Кисивани получил статус города, нуждающегося в международной защите? 4. Какие здания в этом городе имеют особое историческое значение? 5. В каком состоянии находятся сейчас древние постройки и остатки исторических зданий в г. Килва Кисивани? 6. Какие достопримечательности могут привлечь туристов в этот город? 7. Что нужно сделать, чтобы возросла привлекательность города Килва Кисивани в глазах туристов? 8. Чем примечательно здание, отреставрированное швейцарскими специалистами в г. Багамойо? 9. Какие находки были обнаружены вокруг этого здания во время реставрации? 10. Почему правительство Швейцарии тратит свои капиталы на охрану исторических памятников в Танзании? 11. Какие шаги в этом направлении принимает правительство самой Танзании? 12. Багамойо уже включен в список городов, чьи достопримечательности находятся под охраной ЮНЕСКО?
4. Переведите и перескажите на суахили следующий текст. Выскажите свое мнение по поводу проблемы, поднятой в нем:
Wanafunzi waandamana kupinga matumizi
ya mifuko ya plastiki
Wanafunzi wa shule za sekondari za Dar es Salaam jana waliandamana, ikiwa ni kampeni yao kupinga matumizi ya mifuko ya plastiki, ambayo walisema ni adui mkubwa wa mazingira.
Maandamano hayo, ambayo yaliandaliwa na shirika lisilo la kiserikali, yalianzia shuleni hapo kupitia barabara za Umoja wa Mataifa, Morogoro hadi taasisi ya teknolojia Dar es Salaam (DIT) na kurejea shuleni hapo.
Wakiwa njiani, wanafunzi hao waliwapokonya baadhi ya watu waliokuwa na mifuko ya plastiki na kuwagawia mifuko ya nguo.
Akizungumza baada ya maandamano hayo, mwenyekiti wa shirika hilo alisema zaidi ya shule za sekondari 20 zilishiriki. Wanafunzi hao walihitimisha maandamano yao kwa kufanya mashindano ya kujadili athari za uharibifu wa mazingira na kupendekeza njia gani zitumike ili kuhifadhi mazingira.
Katika kuchangia mada hiyo, wanafunzi hao walishauri elimu ya sayansi na teknolojia itumike ili watu waweze kuelewa athari za uharibifu wa mazingira.
Kwa mujibu wa wanafunzi hao, wananchi wengi wanaharibu mazingira bila kujua na kwamba hali hiyo imetokana na upungufu wa elimu ya sayansi na teknolojia.
5. Раскройте скобки, подобрав на суахили аналитическую глагольную форму, соответствующую данному контексту. Переведите предложения:
1. Tegu (подходил к) rafiki yake Mundula, na huko walitumia wakati wao mwingi katika mchezo wa kutupa mishale kwa kutumia pinde zao. 2. Maskini Tegu (промахивался) alama kila alipoitupa mishale yake. 3. Chifu (болел) kwa muda wa miaka mingi. 4. Tegu angaliweza kumsamehe rafiki yake, lakini wavulana fulani ambao (проходили) pale walimcheka pia. 5. Wazazi wake Juma hawakuwa na habari kwamba (он направлялся) mjini Nairobi. 6. Hakustaajabishwa na yale aliyoyaona Kisumu, maana (он уже посещал) mji huo alipokuwa bado shuleni. 7. Alifanya matembezi mjini Kisumu akiwa na wanafunzi wenzake, na pia akiwa pekee, maana mjomba wake (работал) mjini humo. 8. Juma aliyasikiliza kwa makini sana yale ambayo (ему рассказывали) na wakuu wake. 9. Upepo mkali (дул) na sehemu ya tambarare iliweza kuonekana wazi. 10. Mpaka wakati huu Tegu (был охвачен) na hofu hata asijue la kufanya wala asiweze kusema. 11. Wazee wengi walitazamana na kuonyesha kwamba (они были удовлетворены) isipokuwa wafuasi wachache tu wa Mfupa. 12. Baada ya kumaliza ule muda wa miezi sita ambao (он работал) chini ya uangalizi, kampuni hiyo ilimpatia Juma nafasi ya masomo ya juu. 13. (Они питались) matunda ya mwitu, maana walishindwa kula vyura na mijusi. 14. Kwa muda mrefu kidogo Muki alikuwa na furaha kwa sababu (он получал) chakula kingi wala hakuwa na kazi ngumu ya kumsumbua. 15. Mama yake (будучи сердитой) akamjibu, “Ndiyo unaniambia kuwa hukuleta nyama?” 16. Simba (будучи раненым) vibaya sana, alitoweka kwenye majani marefu. 17. Kumbe wakati huo Goja (уже принял решение) kwamba atampeleka Kishosha mpaka afike kwao salama salimini. 18. Wakati huo Tegu (держал) mkuki wake imara kabisa. 19. Macho akaamuru, “Mkamateni Mfupa, na mleteni kwangu. Anastahili kupata adhabu yote. (Когда он уйдет), sote tutakuwa na furaha. 20. Goja, jeraha lake (будучи завязаной) amesimama mbele ya watu.
6. Перескажите следующий текст на суахили, обратив внимание на перевод подчеркнутых выражений:
Приказ вожака
Любопытную картину наблюдал я однажды в джунглях Центральной Африки, куда мы ездили для охоты на диких слонов.
Наша машина ехала по узкой лесной дороге. Справа и слева непроходимой стеной стоял густой тропический лес.
Вдруг нам пересекла путь стая шимпанзе. Одна за другой обезьяны выбегали на дорогу и торопливо уходили в чащу. Я приказал шоферу остановить машину и подождать, пока обезьяны уйдут.
Старый вожак внимательно следил за передвижением своих сородичей. Иногда нам даже казалось, что он каким-то своим способом считает обезьян. Последней на дорогу выбежала маленькая обезьянка, должно быть, сильно напуганная нашим присутствием. Она уже прошла половину дороги, как вдруг старый вожак подбежал к ней и принялся изо всех сил трясти ее, при этом крича ей что-то.
Так он заставил обезумевшую от ужаса обезьяну вернуться обратно в чащу. Через минуту обезьяна появилась снова. На этот раз она была не одна: за ее шею крепко держался шимпанзе-ребенок.
Прыжок вверх – и счастливая молодая мать, прижимая к себе малыша, исчезла в густой зелени тропического леса. Теперь все было в порядке: все обезьяны перешли через дорогу. Крикнув нам на прощанье “хоп-хоп”, старый вожак ушел в чащу леса.
7. Переведите следующий рассказ. Придумайте к нему заголовок и разыграйте его в лицах:
Siku moja shida ilitokea katika nchi fulani. Shida hiyo ilikuwa kiu, na kiu hiyo ilitokea kwa kuwa mvua haikunyesha kwa muda wa mwaka mzima; mito na chemchemi zikakauka, wanawake waliokuwa wakizoea kwenda kuchota maji mitoni na kisimani waliona maji yakipungukapunguka mpaka yakaisha kabisa. Mwisho iliwapasa kwenda na madebe safari kubwa mpaka nchi jirani iliyokuwa na boma la maji. Pale walipata maji kwa kibali cha wenyeji wa nchi hiyo, lakini safari ilikuwa ndefu sana, nao wanawake walisumbuliwa sana hata wakaanza kusemezana na kuulizana, “Kwa nini tunasumbuliwa hivi? Kama watu wa nchi hiyo jirani yetu wanaweza kujisaidia kwa kujenga boma la maji ili wawe na maji wakati mvua hainyeshi, mbona sisi hatuna boma kama wao?”
Mwisho wazee wa nchi iliyo na kiu walikutana ili shauri lifikiriwe. Kukawa na mazungumzo mengi. Wengine walisema, “Mbona twasumbuliwa hivi? Haikosi kiu kutokea mara kwa mara; hii ndiyo hali ya binadamu hapa duniani. Tusipojaliwa mvua na Mungu, basi tuvumilie. Kuchota maji ndiyo kazi ya wake zetu, waache kelele zao!” Wengine wakakataa hayo wakisema, “Sivyo kabisa. Kweli Mungu ndiye aliye mwanzo wa yote, lakini ametupa akili, na kukiwa na njia ya kuepukana na shida hiyo ya kiu inayoleta matata katika nyumba zetu tujaribu kujisaidia. Hali ya binadamu siyo kukaa tu bila ya kutumia akili zetu. Tupeleleze shauri hilo la boma la maji.”
Baada ya mazungumzo mengi walipatana kwamba ni lazima wajenge boma la maji, wakapata msaada wa namna nyingine kutoka kwa serikali, raia wote wakaitwa, kazi ikaanza.
8. Сделайте письменный перевод текста:
Wizara yatakiwa kukabili uvamizi
wa wanyamapori
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ametoa wito kwa wizara ya maliasili na utalii kusaidia juhudi za kukabiliana na uvamizi wa wanyamapori kwenye mashamba ya wakulima.
Akizungumza hivi karibuni baada ya kutembelea mashamba yaliyoharibiwa na wanyamapori wilayani humo mkuu wa mkoa alitaka wahusika katika wizara hiyo kutembelea maeneo hayo kujionea uharibifu uliojitokeza.
Baadhi ya maeneo ya kilimo na malisho ya mifugo yanayomilikiwa na wawekezaji wakubwa yamevamiwa na wanyamapori wilayani Siha ambapo wameharibu miundombinu ya malisho na mashamba yaliyolimwa ngano.
Akizungumzia athari hizo mmoja wa wawekezaji kwenye mashamba hayo alisema wanalazimika kuhamisha mifugo yao kuepusha hasara zinazoweza kujitokeza.
Wanyama jamii ya nyumbu, pofu, pundamilia na swala wanaotoka katika mbuga ya Amboseli nchini Kenya, wamekuwa wakivamia mashamba ya wakulima na wawekezaji wa sekta ya kilimo wilayani Siha na kuharibu miundombinu ya ufugaji.
Imeelezwa kuwa wanyama hao walianza kuvamia mashamba hayo katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita na kusababisha hasara kubwa, na pia kuzuia wakulima kuandaa mashamba yao kwa msimu mpya wa kilimo.
Uvamizi wa wanyamapori kwenye mashamba unatokana na uhaba wa watumishi katika kudhibiti hali hiyo, hivyo kuilazimisha wizara husika kuweka vituo vya askari wa wanyamapori katika kanda maalumu jirani na sehemu zenye matatizo.
9. Переведите:
- Уганда не желает стоять в стороне в развитии туристического бизнеса и всячески стремится сохранить свою притягательность в качестве "жемчужины Африки", как когда-то ее назвал Уинстон Черчиль, первым посетивший эту страну еще в 1907 году.
- Главный управляющий заповедника Мкомази рассказал корреспондентам об интересном эксперименте по ввозу к ним носорогов редчайшего вида, закупленных в ЮАР. Этот проект, направленный на улучшение заповедника, проводится под покровительством Международного Фонда охраны диких животных.
- Главным врагом носорогов являются браконьеры, которые не останавливаются даже перед электрическими заграждениями в поисках дорогостоящего рога этого животного.
- Правительство Занзибара постановило осуществлять строгий контроль за охотой на антилоп, поголовье которых стало резко сокращаться, и ограничило срок охоты на этих животных до 6-ти месяцев в году.
- В некоторых районах Танзании слоны стали реальной угрозой для местных жителей, поскольку они начали регулярно вторгаться на их поля и уничтожать посевы и урожаи.
- По оценкам специалистов нужны дополнительные меры для привлечения инвесторов в туристический сектор экономики.
- Гора Килиманджаро стала национальным парком в 1973 году. Непрекрашающийся с тех пор поток туристов наносил природе большой вред – на склонах оставались тонны мусора. Сегодня, к счастью, эта проблема уже решена.
- Основная роль национальных парков Танзании заключается в охране дикой природы. 14 парков были созданы для того, чтобы сохранить природные богатства страны и обеспечить благоприятную среду для процветания флоры и фауны.
10. Переведите и перескажите следующий текст:
Wanawake wa pwani ya Afrika ya Mashariki hupenda sana kutumia maua. Hutumia maua wakiwako nyumbani mwao. Wakienda arusini, karamuni au kwenye sherehe fulani pia hutumia maua, yaani hutumia maua wakati wa furaha, si wa msiba au huzuni.
Maua hutungwa pamoja na hupachikwa nyweleni kama pambo. Maua yanayotumiwa ni kama yasmini, nargisi, mawaridi na mengine. Hutungwa pamoja katika uzi. Maua haya pengine hutiwa ndani ya kabati la nguo ili nguo zilizomo humo zinukie vizuri zinapovaliwa.
Kati ya maua yanayopendwa sana kwa ajili ya harufu yao nzuri ni nargisi. Maua haya yananukia vizuri ajabu. Wanawake huyapachika nyweleni. Kuna maua mengine maarufu ambayo mwanamke aliyejipamba kwa maua haya akipita njiani hujulikana mara moja kwa vile yanavyotoa harufu nzuri.
Maua yenye kutoa harufu nzuri hutungwa pamoja na nargisi na yasmini kutengenezea koja la maua. Koja hili huvalishwa bwana na bibi arusi; pia mgeni wa heshima anapohudhuria sherehe au mkutano.
Wanawake huyapataje maua haya? Maua haya huuzwa barabarani nyakati za jioni. Vile vile huzungushwa mitaani na wanawake huyanunua. Baadhi ya wanawake wanazo bustani zao ndogo karibu na nyumba zao au ndani ya nyua za nyumba zao. Humo mabustanini hupandwa miti ya maua kama yasmini, nargisi na mawaridi ambayo hutunzwa sana ili imee vizuri.